Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Chama Cha Mapinduzi(CCM),Mkoa wa Mwanza, kinatarajia kuzindua kampeni za chama hicho ngazi ya Mkoa Agosti 29,2025, huku mgombea Mwenza wa kitu cha Urais Dkt.Emmanuel Nchimbi akiwa mgeni rasmi.
Huku wananchi na wanachama wa CCM Mkoa wa Mwanza wakiombwa kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa kampeni hizo ili kusikiliza sera kutoka kwa wagombea wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 27,2025,Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Omary Mtuwa, amesema Mkoa huo kichama umepata bahati ya kuwa Mkoa wa pili kuandaa kampeni, ambapo Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais ndiye atakayezindua kampeni hizo zitakazofanyika uwanja wa Furahisha,uliopo wilayani Ilemela.
Mtuwa amesema,CCM wamejiandaa vyema kushiriki kampeni katika Mkoa wa Mwanza huku vipaumbele vyote walivyonavyo vipo katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa chama hicho.
“Wananchi watarajie kampeni zitakazofanyika Mwanza zitakuwa za kistaarabu,za mfano, zitakazonadi sera na kueleza namna serikali yake itafanya katika kipindi cha miaka mitano,”amesema Mtuwa.
Pia amewasihi watia nia wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho walijitokeza lakini hawakufanikiwa katika kura za maoni kuungana na kuvunja makundi.
“Kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama chetu,makundi yalishaisha Agosti 22,2025 baada ya uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Ubunge na Udiwani.Sasa ni kundi moja la CCM,tuungane kuhakikisha chama chetu kinashinda,”.

More Stories
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro
LGTI wanawake waadhimisha siku yao Ngorongoro