*Hadi Agosti 19, vyama vya siasa 11 vyajitokeza
Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Wagombea Ubunge Jimbo la Ilemela kupitia vyama mbalimbali vya siasa, wameendelea kujitokeza kuchukua fomu za uteuzi wa nafasi hiyo katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo mkoani Mwanza.
Ambapo Agosti 19,2025 wagombea Ubunge wawili ambao ni Asteria Laurent Masunga kutoka chama cha UPDP na Faustine Barnabas Sonda kutoka chama cha ADA- TADEA, wamechukua fomu za uteuzi wa nafasi hiyo katika Jimbo la Ilemela ambazo walikabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo Herbert Bilia.
Wagombea hao wawili wameungana na makada wengine tisa wa vyama vya tofauti vya siasa katika mbio za kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo hilo.
Hivyo kufanya idadi ya wagombea ambao wamechukua fomu toka zoezi hilo kuanza hadi Agosti 19,2025, kufikia 11 kutoka vyama mbalimbali vya siasa jimboni humo.
Mbali chama cha UPDP na ADA- TADEA vyama vingine ambavyo vimechukua fomu jimboni humo ni pamoja na CHAMA MAKINI , UMD, CCK, AAFP,DP,NLD,SAUTI YA UMMA, N.R.A na ACT WAZALENDO,
Kwa mujibu wa kalenda ya matukio kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025 zoezi hili litahitimiswa Agosti 27 2025 .

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi