*Vifo hivyo vimetokea katika matukio mawili tofauti
*Mtuhumiwa wa mauajiĀ naye adaiwa kuuwawa na wananchi
Judith Ferdinand, Timesmajira Online-MwanzaĀ
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi wa matukio mawili tofauti ya mauaji yaliyosababisha vifo vya watu wanne vilivyotokea wilayani Nyamagana mkoani Mwanza kwa nyakati tofauti.
Alizy mkoani hapa,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,DCP.Wilbod Mutafungwa,amesema,katika tukio la kwanza Agosti 8,2025 majira ya saa 05:00 usiku, mtaa wa Kasulu Kata ya
Isamilo, wilayani Nyamagana, Ibrahim Ramadhan(30),mkazi mtaa wa Cheo, mkoani Tabora,anadaiwa kuwashambulia watu wawili kichwani na sehemu mbalimbali za miili yao kwa kutumia nyundo na kusababisha vifo
vyao baada ya kuvuja damu nyingi.
Mutafungwa amewataja Walioshambuliwa kuwa ni Rubera Masood na Kudra Almas,wote ni wafanyabiashara na wakazi wa mtaa wa Kasulu, kata ya Isamilo, Wilaya ya Nayamagana.
“Inadaiwa kwamba mnamo Agosti 02,2025,mtuhumiwa ambaye ni Ibrahim,alifika nyumbani kwa Ustadhi Juma Idd, mganga wa tiba asilia anayeishi, mtaa wa Kasulu,kwa ajili ya kupata tiba.Ilipofika Agosti 08,2025 majira ya saa 05:00 usiku,mgonjwa huyo alichukuwa nyundo iliyokuwa
ndani ya chumba alichokuwemo na kuanza kuwashambulia watu kisha kuwaua watu hao ambao walikuwa ni wasaidizi wa karibu na ndugu wa mganga,”amesema Mutafungwa.
Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alijaribu kutoroka lakini wananchi waliokuwa na hasira walimkamata na kumshambulia kwa mawe na silaha za jadi.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi lifika eneo la tukio na kumnusura mtuhumiwa huyo ambaye kwa wakati huo
alikuwa na hali mbaya kiafya na kumpeleka Hospitali ya Mkoa Sekou-Toure kwa matibabu zaidi lakini kwa bahati mbaya alifariki wakati anapatiwa matibabu.
Amesema,miili ya marehemu wote watatu imehifadhiwa hospitalini kwa uchunguzi wa kitaalam huku uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea.
“Kwa sasa tunamshilikia Ustadhi Juma
Idd, mganga wa tiba asilia na tunaendelea kumhoji kuhusiana na tukio hili,”amesema Mutafungwa na kuongeza
“Tunatoa wito kwa waganga wa tiba asilia kuchukua tahadhari kwa
wagonjwa wanaowapatia huduma kwa kutambua historia zao kiafya, kuwashauri na kuwaelekeza wagojwa wenye magojwa wasiyoweza kuyatibu kwenda hospitali kupata tiba za kitaalam zaidi kulingana na magojwa yao,”.
Haya hivyo Mutafungwa amesema,katika tukio linguine limetokea Agosti 09,2025 majira ya saa 2:50 asubuhi, mtaa wa Malimbe, Kata ya Luchelele wilayani Nyamagana, kando ya barabara ya Luchelele,ulionekena mwili wa kijana mmoja, jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati
ya miaka 25 hadi 30 akiwa ameuawa huku mwili wake ukiwa na majeraha mikoni na shingoni
Mutafungwa amesema,wanaendelea na uchunguzi huku akiomba mwenye taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo aziwasilishe kwa Jeshi hilo,viongozi wa serikali au vyombo vingine vya usalama ili waweze kuzifanyia kazi kwa
haraka na kuwabaini waliohusika na mauaji hayo.
“Mwili wa marehemu ambaye bado
haujatambuliwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa uchunguzi zaidi,”.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako