Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Tabora
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magahraibi imepongezwa kwa kuwafikia wakulima na wafugaji na kuwapa elimu ya fursa mbalimbali za kuwaongezea kipato na thamani shughuli zao.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Balozi Simon Sirro,Agosti 8,2025, alipotembelea banda la EWURA wakati wa kilele cha maonesho ya Wakulima Nane Nane kwa Kanda ya Magharibi,iliyojumuisha mikoa ya Tabora na Kigoma,yaliofanyika mkoani Tabora.

Balozi Sirro,ameeleza kufurahishishwa na ushiriki wa EWURA ambao umekuwa chachu ya upatikanaji wa huduma za nishati na maji mchini,huku akiipongeza kwa kuwafikia wakulima na wafugaji na kutaka utaratibu huo uendelee.
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Walter Christipher, amesema zipo fursa za wakulima kuwekeza kwenye vituo vya mafuta maeneo ya vijijini ili kusogeza huduma kwani uhitaji wa huduma hiyo ni mkubwa.
Pia amesema kuna fursa ya kujisajili kwenye kanzidata ya watoa huduma inayoratibiwa na EWURA ili kutoa huduma mbalimbali katika miradi mikubwa ya nishati na gesi asilia nchini.
“ Katika maeonesho haya, tumewasisitiza wakulima na wafugaji kuzichukua fursa kama za kujenga vituo vya mafuta vijijini baada ya kuuza mazao na mifugo, lakini pia kujisajili kwenye kanzidata, ili washiriki kutoa huduma katika miradi ya kimkakati nchini ya mafuta na gesi asilia mathalani mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongeani Tanga,”amesema Mha.Walter.

Sanjari na hayo ameeleza kuwa,washiriki wa maonesho hayo wamesisitizwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kutunza afya na mazingira,pia kuwekeza katika biashara ya usambazaji wa gesi ya kupikia (LPG),ambapo EWURA hutoa vibali na leseni kuwezesha shughuli hiyo.


More Stories
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro
LGTI wanawake waadhimisha siku yao Ngorongoro