March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PSSSF  yapokea wananchi kwa mwitikio mkubwa Nane Nane 

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),umesema utahakikisha unatoa huduma bora na kuzalisha huduma mpya kila kukicha ili kuongeza thamani kwa wanachama wao.

Huku katika maonesho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane,kwa Kanda ya Ziwa Magharibi yaliofanyika Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza,kumewa na mwitikio mkubwa wa wananchi waliotembelea banda la PSSSF kwa ajili ya kupata elimu mbalimbali.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki,CPA.Rajabu Kinande,akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane kwa Kanda ya Ziwa Magharibi yaliofanyika Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza

Hayo yameelezwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki,CPA.Rajabu Kinande,wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda lao,Agosti 8,2025 katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane.

“Mwitikio umekuwa mkubwa,na matarajio yetu maonesho kama haya ya  Nane Nane,Mei Mosi na yoyote ambayo yanaweza kuwakutanisha wadau wetu, sisi tupo tayari kushiriki kuhakikisha tunawafikishia huduma karibu,amesema CPA.Kinande na kuongeza:

“Mfuko utaendelea kutoa huduma ,bora na kuhakikisha kila kukicha tunakuwa pamoja na  kuongeza bidhaa(products)  mpya ambayo itatumika kuongeza thamani wanachama wetu,”.

Ofisa Matekelezo wa PSSSF Alex William( kushoto),akimsikiliza mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda lao kwenye maonesho ya wakulima Nane Nane kwa Kanda ya Ziwa Magharibi yaliofanyika Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza

Kwa upande wake mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho hayo,Nyamwiza Lucas,amesema,amefanikiwa kupita katika banda la PSSSF na kujifunza kuwa sasa mfuko huo kwa njia ya kidijitali.