Na Heri Shaaban, Timesmajira Online-Dar-es-Salaam
HALMASHAURI ya Jiji la Dar-es-Salaam kipitia Idara ya Elimu Msingi, wamegawa vifaa vya kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule zilizopo wilayani Ilala.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Elimu Msingi na Awali wa Halmashauri hiyo,Magreth Macha, amesema Wilaya ya Ilala ina shule zaidi ya 100 kati hizo shule zenye wanafunzi wa mahitaji maalum zipo 18.
Macha,amesema vifaa hivyo walivyogawa lvimetoka Serikali Kuu kwa ajili ya wanafunzi wa Wilaya ya Ilala wenye mahitaji maalum ikiwemo wa shule ya Uhuru Mchanganyiko,Buguruni Malapa,Mzambarauni na Chanika.
Pia ametoa wito kwa Walimu Wakuu wa shule hizo kutunza vifaa hivyo na vitumike kwa madhumuni yaliokusudiwa .
Huku akiitaka jamii yenye watoto wenye mahitaji maalum wasikae nyumbani badala yake wawapeleke shule wapate fursa ya kusoma elimu bila malipo.

More Stories
Senyamule:Serikali inapaswa kuzitambua Kampuni zinazofanya biashara ya ardhi
Serikali kuendelea kupanua fursa elimu Singida
Kumekucha CDF Cup 2026, NMB yaweka Sh milioni 150