Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa wito kwa wakulima na wavuvi kutumia taarifa za hali ya hewa ili kuleta tija na kuongeza kipato. Wito huo umetolewa kwenye Maonesho Nanenane 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Dole Kizimbani, Zanzibar.
Mkurugenzi wa TMA Ofisi ya Zanzibar,Masoud Makame Faki, akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Banda la TMA aliwahimiza wakulima na wavuvi kufuatilia utabiri wa kila siku, utabiri wa msimu pamoja na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazotolewa na Mamlaka,kwani mkulima hawezi kupata utajiri au ongezeko la pato bila kutumia taarifa za hali ya hewa.
Kaulimbiu ni “Kilimo ni utajiri, Tunza Amani, Lima kwa ubunifu”.



More Stories
Mahundi ahimiza wanawake kutumia kuinua uchumi
Samia aitunuku NMB kwa gawio kubwa Serikalini
Serikali yambana mkandarasi kituo cha umeme Hale