
Na Joyce Kasiki,Timesmajira ,Dodoma
MAMLAKA ya Ufundi na Ufundi Stadi (VETA) imekuja na Teknolojia ya Kilimo bila kutumia dawa za viwandani kwa ajili ya kutunza Afya za walaji .
Akizungumza Agosti 4,2025 katika maonyesho ya wakulima na wafugaji katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma,Mwalimu wa zana za Kilimo na Kilimo bila kutumia dawa za viwandani Kutoka VETA Kihonda mkoani Morogoro Gema Ngoo amesema,wamekuja na Teknolojia hiyo Ili kuwakinga Watumiaji wa bidhaa za Kilimo hasa mbogamboga dhidi ya magonjwa.
“Sisi tunatengeneza mbolea ya Busta kwa kutumia uchafu wa vyakula pia tunachanganya kwenye udongo wenye rutuba pamoja na minyoo.”amesema Ngoo
Amesema wametengeneza bustani inayotembea kwa ajili ya kuoanda mboga mboga ambapo makopo hutumija kwa ajili ya kupandia.
Akizungumza faida ya mbolea hiyo Ngoo amesema ni salama kwa Afya ya binadamu lakini pia ni rahisi kutumia.
“kama nikivyosema awali,mbolea pamoja na dawa zetu za kufukuza wadudu tunatengeneza kwa njia za asili tofauti na zile za viwandani kwa hiyo faida yake kubwa za matumizi ya bidhaa zetu ni Usalama hasa wa kiafya.”amesema Ngoo
Ametaja faida nyingine
inapatikana kiurahisi na hutumika katika maeneo madogo ya nyumbani lakini pia gharama ni nafuu
Aidha amesema mbolea hiyo inapatikana VETA Kihonda mkoani Morogoro.
Amewaalika Wadau wote kufika maonyesho ya Nane Nane Banda la VETA kujionea namna vijana na walimu Kutoka chuo hicho wanavyobuni bidhaa mbalimbali zinazoenda kutatua changamoto katika jamii.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi