Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
TANZANIA imesema ipo tayari kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za akili unde ikiwemo mifumo, pa moja na miundombinu itakayo linda faragha na usalama wa taarifa binafsi wakati wa matumizi ya akili unde
Akiwakilisha Serikali ya tanzania katika jukwaa la kwanza la wadau wa akili unde lililofanyika hapa nchini, likihusisha watalaamu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Uingereza, Ujerumani na mataifa jirani ya afrika mshariki, Mkurugenzi wa Tume ya Tehama, Dkt. Nkundwe Masaga, amesema, utayari huo unakuja kwa kuweka sera na kanuni ambazo zitalinda usalama na faragha ya data na taarifa binafsi za watumiaji wa akili unde.
“Katika kuhakikisha teknolojia inakuwa, inabidi kuwepo na sera na kanuni zitakazowezesha kulinda usalama wa faragha na taarifa binafsi za watu ambao watakuwa wanatumia akili unde” alisema Nkundwe.
Kwa upande wake, Yusuph Kileo, mtaalamu wa masuala ya usalama mtandaoni amesema, utayari kwa nchi ya Tanzania katika matumizi ya akili unde una chagizwa na ujio wa mkakati na miongozo itakayo linda maadili ya mtanzania katika matumizi ya akili unde
Nao baadhi ya washiri wa mkutano huo wamesema, jukwaa la akili unde litasaidia wadau hao kupata maarifa na kuja na mikakati ikiwemo mapendekezo ya uwepo wa sheria na kanuni kwa ajili ya kusimamia matumizi ya akili unde hususani katika ongezeko la matumizi ya simu janja na intaneti nchini
Aidha, katika hatua nyengine pembeni ya jukwa la akili unde Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urusi, zimesaini makubalino ya ushirikiano katika sekta ya tehama pamoja na kukuza uchumi wa kidigitali.
Baada ya kukamilika kwa Serikali hizo kutiliana saini za makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Tume ya Tehama, Dkt. nkundwe Masaga pamoja na Mwakiliahi wa Serikali ya Urusi Anayeshughulikia Masomo kwa Nchi za Afrika, Andrey Maslov, wamesema ushirikiano huo utawezesha mafunzo, ufanyaji tafiti na kuendeleza sekta ya teknolojia ili kukuza pamoja na kuendeleza jitihada za Serikali ya tanzania katika kukuza uchumi wa kidigitali.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako