Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempitisha Andrew Magombana , kujumuishwa kwenye orodha ya wagombea wa nafasi ya ubunge Jimbo la Ulanga, mkoani Morogoro, katika mchakato wa ndani ya chama.
Magombana ni miongoni mwa wagombea sita waliopitishwa kushiriki kura za maoni ndani ya CCM kwa jimbo hilo.

Wagombea wengine wanaowania kuteuliwa na CCM kuwania ubunge Jimbo la Ulanga ni pamoja na Salim Hasham , Abdallah Kirungu, Thabiti Dokodoko, Christina Mpete pamoja na Agustino Matefu.
Akitangaza majina hayo Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amesema kuwa uteuzi wa majina hayo umetokana na uchambuzi makini, kwa kuzingatia uadilifu, uwezo wa uongozi na kukubalika kwa wagombea miongoni mwa wananchi.

More Stories
TISEZA Songea kuvutia uwekezaji, ajira zaidi zapatikana
Serikali yajipanga kukabiliana na athari za El Nino
Wadau watakiwa kushirikiana Kuhifadhi Ziwa Tanganyika