March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bituro Kazeri achukua fomu kuomba ridhaa kugombea ubunge Jimbo la Mwibara

Fresha Kinasa TimesMajira Online Mara. 

KADA wa Chama Cha Mapinduzi Bituro Kazeri amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mwibara Wilayani Bunda Mkoani Mara.

Bituro amechukua fomu hiyo Julai Mosi, 2025, ambapo alikabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda Evodia Edward. Ambaye amemtakia heri katika kinyang’anyiro hicho. 

Amesema kuwa, kilichomsukuma kugombea nafasi hiyo ni kutaka kushiriki kikamilifu katika utatuzi wa changamoto za Wananchi na kutekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi kwa ufafanuzi. 

Aidha, Mtia nia huyo amepongeza mchako wa uchukuaji fomu ndani ya chama Cha Mapinduzi katika Wilaya ya Bunda.