Na Mwandishi wetu,Timesmajira
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Lameck Nyambaya amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Jimbo la Segerea Kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Nyambaya amechukua fomu mapema leo Juni 1,2025 na kukabidhiwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, Sylvester Yeredi .
Nyambaya amesema ameamua kutumia haki yake ya kikatiba kwa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea jimbo la Segerea kutokana na kuwa na uwezo, pamoja na kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kazi ambazo amekuwa akizifanya .
” Nimeamua kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Jimbo la Segerea”amesema Nyambaya



More Stories
MD Twange atoa onyo kwa wezi wa miundombinu ya umeme
WRRB yaanza uimarishaji mfumo stakabadhi za ghala
Senyamule:Serikali inapaswa kuzitambua Kampuni zinazofanya biashara ya ardhi