Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaonya Makatibu na Watendaji wa chama hicho, kutowatoza fedha zaidi za kiwango cha gharama ya uchukuaji fomu wanachama wanaojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi za Ubunge na Udiwani.
Onyo hilo limetolewa jijini Dodoma na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA. Amos Makalla alipozungumza na waandishi wa habari,ambapo onyo hilo limekuja baada ya kupatikana kwa taarifa kuwa, kuna baadhi ya watendaji kudaiwa kuwatoza wanachama fedha zaidi ya kiwango kilichowekwa cha ada ya fomu.
Ambapo gharama ya uchukuaji wa fomu ni ni shilingi 500,000 kwa nafasi ya Ubunge huku nafasi ya Udiwani ikiwa ni shhilingi 50,000.

More Stories
Mfanyabiashara,vibarua mbaroni wakituhumiwa kuchimba mahandakiÂ
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8