March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mosoud Mapande achukua fomu kuomba ridhaa kugombea jimbo la Kivule

Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,Dar

MTAALAMU wa Masuala ya Uchumi na Fedha kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mosoud Mapande amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mapande amechukua fomu mapema leo Juni 29,2025 na kukabidhiwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Sylvester Yeredi

Amesema endapo atapitishwa atahakikisha anamsaidia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo.