March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Nyansika aeleza mafanikio kata ya Kivule

Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar

DIWANI wa Kata ya Kivule Wilayani Ilala, Nyansika Getama, aeleza Mafanikio yake ndani ya kata Kivule kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi(CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo Juni 19,2025  Nyansika amesema baadhi ya mambo aliyotekelezwa katika kipindi chake ni kujengwa hospitali ya kisasa ya wilaya ambapo katika hospitali hiyo ya wilaya baadhi ya majengo yaliojengwa Jengo la upasuaji,jengo la wodi ya wanaume,jengo la wodi ya wanawake jengo la Monchwari,kuchoma taka na jengo la macho na meno.

Aidha amesema kuwa katika hospitali hiyo huduma za upasuaji ,X-Ray,ultrasound  zinatolewa na hivi karibuni wamepokea  shilingi bilioni 5 kwa ajili ya Wodi ya watoto,Wodi ya wanaume na Wodi ya kinamama ambapo amesema zote hizo ni juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

“Ndani ya kata ya kivule naishukuru Serikali kwa kuleta maendeleo makubwa sekta ya Elimu Sekondari Serikali imefanikiwa kujenga  shule tano za Sekondari ukiwemo Abuuy Juma,Kivule,Misitu na Kerezange na katika uongozi wangu utekelezaji wangu wa Ilani nimefanikisha kwa kujenga Sekondari mpya vyumba 22 na kupelekea high school,”Nyansika.

Akizungumzia sekta ya elimu msingi amesema kutokana na ukubwa wa kata hiyo mpaka sasa Kivule ina shule ya Msingi Kivule,shule ya Msingi Serengeti,shule ya Msingi kivule Anex na shule ya msingi Bombambili.

Diwani Nyansika akizungumzia mikopo ya Serikali ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri ya vijana na watu wenye ulemavu imetolewa kwa vikundi vilivyopo ndani ya kata hiyo na sasa hivi vikundi vingine vipo katika utaratibu wa kupewa mikopo ya Serikali ambayo aina riba

Akizungumzia masoko amesema  kwa sasa Kivule kupitia mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP awamu ya pili watajenga masoko mawili Kivule na Kerezange wafanyabishara wa kata ya Kivule  watafanya biashara zao katika kata hiyo kwa ajili ya kukuza uchumi katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Akizungumzia mikakati yake ndani  ya kata ya Kivule kujenga shule ya mchepuo wa Kingereza sh,560,000,000 kujenga
shule mpya ya msingi magole A kujenga ujenzi wa masoko ya kisasa pamoja na barabara   fremkumi kiwango cha  lami.

Alisema mikakati mingine kujenga barabara ya  fremukumi  njia nne kiwango  cha lami  Chuo cha wauguzi , Mabweni ya wanafunzi wa chuo  cha wauguzi mawili  ya kike na ya kiume, Umaliziaji wa ofisi ya mtaa wa Bombambili na  Ufidiaji wa maeneo ya kwa Fedha na Magole A.