Na Stephen Noel,Mpwapwa .
Wakazi wa Kijiji cha Chilendu kata ya Rudi wilaya ya Mpwapwa wamefurahia Huduma za upasuaji Katika Kituo chao cha Afya baada ya kusubiri Huduma hiyo Kwa miaka hamsini Sasa.
Wakiongea kijijini hapo baadhi ya Wananchi hao wamesema ilikuwa inawalazimu kusafiri umbali wa kilomita 45 Hadi tisini na Tano kutafuta Huduma hizo Katika Kituo cha Afya kibakwe au hospitali ya wilaya huku pia changamoto za Miundo mbinu na makorongo hasa kipindi cha mvua kuwa kikwazo kingine na wakati mwingine kusababisha vifo vya watoto na akina mama wajawazito wakiwa wanasubiri Maji yapungue na kumvusha mgonjwa.
Diwani wa kata hiyo Peter Mwikanu amesema ujenzi wa jengo Hilo la pasuaji lililogharimu zaidi ya million miatano ni ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Korea kusini.
Aidha amesema zaidi ya wakazi i ya wakazi elfu arobaini wanategemea kunufaika na Huduma hizo hasa Kwa vijiji vinavyo izunguka kata hiyo na kata za jirani kama Manga’aliza.
Kwa upande wake mganga Mkuu wa Halmashauri Dr.Stanley Mlay amedai kuwa baada ya maboresho makubwa ya sekta ya Afya ni kuhamikisha Kila kata inakuwa na Kituo cha Afya kinachotoa Huduma za upasuaji Kwa lengo la kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Naye Mganga mfawidhi wa Kituo hicho Dr.Ambilekisye Kajange amesema kabla ya Huduma hizo kuanza kutolewa tangu kilipojengwa mwaka 1975 ilikuwa inamlazimu kuwaandikia rufaa wagonjwa. Kuanzia Kumi na watano Hadi ishirini Kwa mwezi kitu alichosema kilikuwa kinaongeza gharama za uendeshaji wa Kituo.
Mmoja wa madaktari bigwa waliofanya upasuaji wa mala ya kwanza daktari Bigwa wa upasuaji na magonjwa ya akina mama Dr. Denis Mwanampazi amesema Katika kuzindua Huduma hizo wanefanya upasuaji Kwa wazazi watatu na wote wanaendelea vizuri pamoja na watoto wao
Hata hivyo ametoka wito Kwa uongozi wa halmashauri kuendelea kuboresha vitendea kazi Katika chumba hicho cha upasuaji.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako