Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya
BAADHI ya wagonjwa na baadhi ya mali katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wamenusurika na kuungua moto baada ya majengo mawili ambayo ni wodi ya watoto na wazazi kuwaka moto leo mchana, huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.
Akizungumza na TimesMajira wakati akiwa katika eneo la tukio Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta amesema wamefanikiwa kuokoa wagonjwa na baadhi ya samani na vifaa tiba vya hospitali hiyo.
“bado chanzo cha moto hakijafahamika na japo tumefanikiwa kuokoa wagonjwa, na baadhi ya samani na vifaa tiba vya hospitali hiyo.” Amesema Mkuu wa Wilaya Claudia Kitta

More Stories
TMA yaeleza faida taarifa hali ya hewa
Wananchi wapata elimu ubora,usalama na bidhaa
Mkomi Aridhishwa na Utendaji wa PSSSF