Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,
Nkasi
Umoja wa Watumishi Nkasi (UWANKA),umepata viongozi wa mpito watakaouongoza umoja huo kwa kipindi cha miezi sita.
Huku moja ya jukumu walilonalo ni kujenga umoja huo na kuweka misingi itakayotumika kuandaa uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba na kupata viongozi wa kudumu.
Waliochaguliwa ni Mwenyekiti Didas Saadan,Makamu Mwenyekiti Beatrice Mlay,Katibu mtkuu Victor Makoba na Mweka Hazina Abbas Kiloge.

Kwa mujibu Ofisa Utumishi wa Halmashauri Wilaya ya Nkasi,Rainel Mwenda,kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Afraha Hassan, amesema dhumuni la umoja huo ni kusaidiana wakati wa shida pamoja na kuleta ushirikiano mahala pa kazi.
Mwenda amedai kuwa umoja huo kama utakwenda sawa na malengo waliyoyaweka huenda wakaenda mbali zaidi kwa kutengeneza ushirika wenye nguvu utakaokuwa mfano wilayani Nkasi na mkoa kwa ujumla.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako