May 29, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Coca-Cola ‘chupa la machupa’ yapeleka ladha mpya Forodhani, Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KAMPENI ya Coca-Cola ‘Chupa la machupa’, imeamua kupeleka ladha mpya Forodhani, katika Kisiwa cha Zanzibar, ambapo ni sehemu maarufu kwa vyakula vya baharini.

Eneo hilo la fukwe lililope kwenye Mji Mkongwe, hufurika harufu ya vyakula vya kukaangwa, mazungumzo, na msisimko wa watu wanaokusanyika pamoja kufurahia ladha mbalimbali.

Kwa kutambua suala hilo, Coca-Cola imejiunga rasmi na utamaduni huo kupitia kampeni yake ya Chupa la Machupa kusheherekea ladha, utamaduni, na muunganiko wa kijamii, inayonogesha msisimko mpya katika mojawapo ya vivutio maarufu vya chakula Zanzibar.

Pia, eneo hilo, lililo katikati ya Jumba la Makumbusho na Ngome Kongwe, huchangamka zaidi mida ya jioni lenye shamrashamra, ambapo wakazi wa Zanzibar pamoja na watalii hukusanyika kufurahia vyakula vya baharini kama pweza, kamba, kaa, ngisi na barracuda.

Vyakula vingine vya mtaani ni kama urojo, sambusa, kahawa ya viungo, mihogo, ndizi za kukaanga, viazi vitamu hadi pizza maarufu ya Zanzibar.Forodhani inatoa zaidi ya chakula, ni eneo linalo sheherekea utamaduni.

Watembeaji hujipatia nafasi kutembea kandokando ya bahari, kuketi kwenye benchi au ukingo wa ukuta wa bahari na kufurahia upepo mwanana pamoja na mandhari ya kuvutia ya bahari ya Hindi.

Chakula cha Forodhani kinaakisi historia ya Zanzibar kama kitovu cha tamaduni mbalimbali. Mchanganyiko wa ladha za Kiarabu, Kihindi na Kimediterrania, zilizopikwa kwa viungo adimu kama masala, hiliki, kitunguu saumu.

Vilevile, manjano na zafarani, huenda vizuri sana na vinywaji baridi kama Coca-Cola, Sprite, Fanta Orange, Fanta Pineapple au Fanta Passion.

Kupitia kampeni ya Chupa la Machupa, Coca-Cola inaleta furaha kupitia chupa yake maarufu ya glasi ya 350ml kwa punguzo la bei.

Chini ya kila kizibo cha chupa, wateja wanaweza kupata zawadi mbalimbali ikiwemo kinywaji cha bure kabisa, punguzo la asilimia 70 (TSh 200) au asilimia 30 (TSh 500). Coca-Cola huwalipa wauzaji moja kwa moja, ili kuhakikisha mteja anaendelea kufurahia soda yake bila bugudha.

Kwa wale watakaokosa kuhudumiwa papo hapo kwa sababu ya upungufu wa bidhaa, Coca-Cola imetoa namba ya msaada 0742 633 877 ambapo wateja watapewa maelekezo ya mahali pa karibu pa kuchukua zawadi zao.

Kampeni hiyo ya miezi miwili inalenga kuwafikia zaidi ya watumiaji 100,000 kila wiki, ikiwa ni sehemu ya kuwazawadia wateja waaminifu na wakati huo huo kuimarisha biashara ndogo ndogo kwa kuongeza mauzo na kipato kwa wafanyabiashara wa Forodhani.Lakini Forodhani haihusu tu suala la chakula peke yake.

Eneo lingine ni Makachu, eneo maarufu la baharini ambalo limekuwa alama ya vijana na utamaduni wa pwani ambao hujirusha kuingia baharini. Kianzio chake kikiwa ni mchezo wa kawaida uliokuwa ukijulikana kama Kachumbe, baadaye kuwa Kachu na hatimaye Makachu, eneo hili sasa limekuwa sanaa ya maonesho.

Tangu mwaka 2022, waogeleaji wamekuwa wakirusha mabango yenye majina ya watu maarufu, chapa na wateja, wakiyachomeka kwenye maonesho yao ya baharini.

Coca-Cola pia, ilijiunga na burudani hii kupitia Chupa la Machupa, ambapo waogeleaji waliruka baharini wakiwa wameshika chupa, glasi za Coca-Cola na mabango ya kampeni, tukio lililowavutia wengi na kueneza ujumbe wa furaha ya kampeni hii kwa njia ya kipekee kabisa.

Kwa mujibu wa mashuhuda na wachambuzi wa burudani za mitaani, hiyo ni zaidi ya kampeni, ni njia mpya ya kuunganisha chapa na utamaduni wa watu, bila ya kuharibu asili zao.