May 29, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Machinga wapewe kipaumbele kwenye maeneo ya Biashara

Na Bakari Lulela, Timesmajira

MASOKO ya kimkakati kote nchini, wapewe kipaumbele wafanyabiashara wadogo Machinga katika kufanyia shughuli za kibiashara kwa manufaa yao na serikali kwa ujumla.

Serikali haitarudi nyuma itakuwa bega kwa bega na wamachinga katika kuwabeba kuhakikisha wanatendewa haki na kuondoa unyonge vipindi vyote vya ukombozi dhidi ya kundi hili.

Akizungumza katika kongamano maalumu la Machinga lililofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam mgeni rasmi, waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Mohammed Mchengerwa amesema wako radhi hata kutoa maisha yao viongozi kwa ajili ya kutetea kundi hilo ili taifa lisonge mbele.

“Serikali ipo nanyi hivyo msikubali kuandamana kwa maslahi yao, wakitaka kuandamana waacheni wao pamoja na familia zao Ili kuweza kuwapata vizuri endapo watafanya hivyo,” amesema Dkt Mchengerwa.

Aidha Mchengerwa amesema kuwa kundi hilo liachwe lifanye biashara kwenye mazingira ya amani na salama katika kujilete maendeleo bila kubughudhiwa na lolote ikiwemo Machinga , maafisa usafirishaji na mama lishe.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kuwa Machinga ni kundi maalumu ambalo linahitaji usaidizi wa serikali Ili mipango yao iweze kusonga mbele kimakazi na mipango mbalimbali ya ubunifu wa biashara zao.

Aliendelea kuwa rasimali kubwa ya watu hao wapo ambao ni wabunifu katika kupigania haki kimsingi ya kuinua biashara zao na za wengine lakini pia kufanya biashara wezeshi katika mazingira rafiki na kuweka mikakati dhabiti yenye lengo la kuinua uchumi na maisha yao kwa ujumla .

Naye Mwenyekiti wa Machinga Taifa Steven Lusinde amesema kuwa kundi hilo limejikita kwa maslahi ya wafanyabiashara yenyewe na serikali yao kupitia kwa mama Dkt. Samia Suluhu Hassani pia wameahidi kumpa sapoti kwa kulipa Kodi na kushiriki vema uchaguzi mkuu ambao inatarajia kuwa mwaka huu.