May 29, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mitungi 100 ya gesi yatolewa kwa mama lishe,baba lishe

Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Babati

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara Regina Ndege, amekabidhi majiko 100 yenye thamani ya milioni 5.5, kwa mama na baba lishe wa Kata ya Riroda na Magugu wilayani Babati mkoani humo, ili kuendelea na kuunga mkono matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Ndege amekabidhi majiko hayo kwa walengwa mbele ya Madiwani wa Viti Maalum wa Tarafa ya Mbugwe, Staimili Masasi, Mariam Kwimba pamoja na Naomy Richard.

Ambapo amesema lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye yuko kwenye kampeni ya kuhakikisha asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia kwa usahihi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha amesema anatambua wengi wao mama na baba lishe wamekua wakitumia kuni na mkaa kupikia hali inaweyoweza kusababisha madhara mbalimbali kama macho kuwa mekundu kutokana na moshi pia magonjwa kama kifua kikuuu ama kansa.

Naye Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Mbungwe Naomi Richard, amesema anaamini kupitia wao huyo alitambua makundi maalumu yanayohitaji majiko hayo ilimkuendana na matumizinya kushatibsafi ya kupikia.

Akizungumza kwa niaba ya akina mama lishe Halima Seleman,amesema majiko hayo yatawasaidia kutoka kwenye matumizi ya nishati chafu hadi safi ya kupikia.