Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema licha ya kuwepo Mpango wa kujenga barabara nne katika barabara ya Moshi -Arusha kuanzia Sangisi hadi Maji ya Chai lakini pia upo Mpango wa kujenga lakini pia Serikali inao Mpango wa kufanya matengenezo kwa barabara zilizoharibika ikiwemo ya Moshi -Arusha.
Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo Leo Mei 26 mwaka huu Bungeni jijini Dodoma kufuatia swali la nyongeza la Mbunge wa Arumeru Mashariki Dkt.John Pallangyo ambaye alitaka Mpango wa Serikali wa kujenga barabara ya Moshi -Arusha eneo la Sangisi Hadi Maji ya Chai Kutokana na kuharibika vibaya.
“Barabara ya Moshi-Arusha kuanzia Sangisi hadi Maji ya Chai imeharibika sana ,ni upi Mmango wa Serikali wa kufanyia matengenezo ya haraka barabara hiyo liicha ya kwamba tunafahamu itajengwa kwa kiwango cha njia nne.?”amehoji Dkt.Pallangyo
Akijibu swali hilo,Mhandisi Kasekenya amesema Serikali inao Mpango wa matengenezo ya haraka pale ambapo barabara zimeharibika.
“Naomba nimhakikishie mheshimiwa Mbunge kwamba tumeshaomba pesa kwa Rais na ameshatoa fedha za dharura kwa ajili ya kutengeneza maeneo yote ambayo barabara zimeharibika sana ili wakati tunasubiri ule Mpango kuitengeneza njia nne lakini tuweze kutengeneza maeneo yenye changamoto kubwa hasa barabara aliyoitaja mheshimiwa mbunge”amesisitiza Mhandisi Kasekenya

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako