May 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mchengerwa afurahishwa na utendaji wa Meya Kumbilamoto

Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Ilala

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa,amemtabiriwa mambo makubwa Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti wilayani Ilala mkoa Dar es Salaam kwa utendaji bora wa kazi katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo alisema kungekuwa Jimbo linagawanywa Meya Kumbilamoto angepewa jimbo moja kutokana na kuisaidia Serikali vizuri

Mchengerwa amesema hayo wakati wa kuzindua mradi wa Serikali wa ujenzi wa Soko la nyama choma lililopewa jina la Kumbilamoto mradi huo uliopo machinjio ya Vingunguti wilayani Ilala.

“Nawapongeza Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam mmepata Meya bora Omary Kumbilamoto, mchapa kazi na anafanya kazi kwa weledi za Serikali anajua kazi yake isingekuwa katiba ya chama cha Mapinduzi Meya Omary Kumbilamoto  anapita bila kupingwa na Jimbo lingegawanywa angepewa jimbo moja,”Mchengerwa.

Aidha amewataka madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kumpa ushirikiano Meya Kumbilamoto katika kumsaidi Rais Dkt.Samia  Suluhu Hassan na kusimamia miradi ya maendeleo  vizuri ya Halmashauri.

Wakati huohuo ametoa agizo sheria ibadilishwe kwamba Naibu Meya wa Halmashauri achaguliwe kila baada ya miaka mitano kuanzia sasa sio mwaka mmoja ili kuondoa nongwa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM.

Amemwagiza Katibu Mkuu TAMISEMI kuwasilisha kanuni haraka Bungeni ili aweze kusaini kurekebisha kabla Bunge la Jamhuri ya Muungano kuvunjwa ili iweze kutumika haraka  .

Kwa upande mwingine alimwagia sifa Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya anafanya kazi kubwa katika Wakurugenzi 188 nchini Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam ameshika namba moja anafanya kazi kubwa ya kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kukusanya mapato mengi na kuvunja rekodi.

Akizungumzia suala la amani ya nchi alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuwakamata wote wanaovuruga amani ya nchi kwani katika suala la amani huwezi kuzungumza ukajificha ametaka amani ilindwe kwa nguvu zote kwani yanapotokea machafuko hayaangalii mzee au kijana.

Kwa upande wake Meya Kumbilamoto,amesema sababu ya kujenga mradi huo wa nyama choma ni wafanyabishara kuandamana nyumbani kwake  ambapo awali kulienea uvumi eneo hilo la Serikali limeuzwa ambapo taarifa siyo za kweli.

“Leo mradi wa Serikali umekamilika uliogharimu shilingi bilioni 729.6 fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.Katika mradi huu wa ujenzi wa jengo la soko la nyama choma tunafunga TV kubwa za kisasa kwa ajili ya Wananchi waweze kufatilia matukio mbali mbali ikiwemo taarifa ya habari,”amesema.