Na Bakari Lulela,Timesmajira
WITO umetolewa na wakala wa vipimo (WMA) mkoa wa kinondoni kwa kuwataka watoa huduma za bidhaa kufuata Sheria na taratibu kwa kuuza kwa uwiano sahihi na ubora wa hali ya juu. Kipimo cha kuuza mafuta ni halali mashine ianze kusoma sifuri ndipo inaendelea na tarakimu zingine kwa kupata kilicho bora na sahihi kwa wateja ambao ndio watumiaji.
Akizungumza kwenye kituo cha mafuta cha Engine mikocheni jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya wakiadhimisha ya siku ya vipimo Duniani Kaimu meneja wa wakala hao, Grace Kulegwa amesema watoa huduma wengi hutoa huduma hizo kiholela bila kuzingatia uhalali wa vipimo.
“Tunawataka watoa huduma mbalimbali za bidhaa waweze kupata elimu ya kutosha kuwawezesha kufahamu viwango, ubora na usahihi wa bidhaa wanazozitoa kwa watanzania,” amesema Kulegwa .
Mkuu huyo ameeleza kuwa WMA hujihusisha katika maeneo mbalimbali ikiwemo vituo vya mafuta, afya, mazingira na maeneo ya usafirishaji kwa kuzingatia weledi wa usawa katika kutoa huduma ndani ya jamii ya watanzania.

Aidha WMA mara kwa mara hufanya zoezi la ukaguzi wa kustukiza kwa watoa huduma kubaini namna shughuli mbalimbali zinazofanywa kwa kuzingatia weledi wa Sheria za vipimo.
Hata hivyo kwa wale ambao huenda kinyume na Sheria za vipimo kwa makusudi huchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kulipishwa faini ama kupelekwa kwenye vyombo vya sheria mahakamani.
Kwa upande wake mtoa huduma ya mafuta katika kituo cha Engine cha mikocheni George Hosea amesema kuwa wao kila siku kabla ya kuanza shughuli za uuzaji wa mafuta huanza kwa uhakiki wa vyombo vyao.
Ameeleeza kuwa changamoto zipo lakini wataendelea kuziepuka ili huduma zao ziwe bora na zenye kufuata usawa kulingana na pesa za wateja wao.
More Stories
Zanzibar ipo tayari kupokea wawekezaji wa ndani na nje ya nchi
Elimu ya kilimo tija yawafikia wakulima mikoa mitano.
DCEA yateketeza ekari 157 mashamba ya bangi Kondoa