Na Bakari Lulela, Timesmajira Online
WITO umetolewa kwa waajiri kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria huku wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii wakijua kuwa mfuko wao uko imara na thabiti kuwahudumia.
Akizungumza jijini Dar -es-Salaam Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt.John Mduma, amesema mfuko huo umejidhihirisha kuwa ni chombo muhimu cha ulinzi wa kijamii kwa wafanyakazi nchini na kuahidi kuendelea kuboresha huduma kwa kushirikiana na wadau wote.
“Mfuko huu inatoa ulinzi wa kijamii kwa wafanyakazi wote walioko katika sekta ya umma na binafsi dhidi ya madhara yanayotokana na ajali, magonjwa au vifo vinavyotokea kazini au kutokana na kazi,” amesema Mduma
Aidha Dkt. Mduma amesema kuwa WCF imefanikiwa kuwalipia fidia wafanyakazi na wategemezi wao wapatao 19,650 walipopata ajali, kuugua au kufariki kutokana na kazi ambapo ni hitaji la msingi la uanzishwaji wa mfuko na kuonyesha utendaji wa moja kwa moja kwa wafanyakazi.
Mkuu huyo ameeleza kuongezeka kwa idadi ya mafao hadi kufikia mafao saba makuu ambayo ni pamoja na fao la matibabu, fao la Ulemavu wa muda mfupi, fao la Ulemavu wa kudumu,fao la pensheni kwa wategemezi, fao la wasaidizi wa magonjwa, fao la utengamao na fao la msaada wa mazishi.
Hata hivyo WCF imetekeleza mapinduzi ya kidijitali ambapo zaidi ya asilimia 90 ya huduma zote sasa zinapatikana kwa njia ya mtandao pia mifumo hii imepunguza urasimu, kuongeza uwazi na kuboresha ufanisi wa utendaji kazi.
Ameendelea kuendeleza kuwa Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto chache ambazo mfuko umekuwa ukizifanya kazi kama waajiri kutojisajili na kutowasilisha michango kwa wakati ambapo baadhi ya waajiri bado hawajatekeleza matakwa ya Sheria ya kusajiri wafanyakazi na kuwasilisha michango kila mwezi.
More Stories
Doreen: ‘Msiwafiche watoto wenye utindio wa Ubongo
Serikali yawezesha miradi 80 kwa utaratibu wa PPP
Mpogolo akabidhi Cheti kwa wahitimu