Na Angel Kazinja, TimesMajira, Morogoro.
MKAZI wa Kijiji cha Madizini Kata ya Mtibwa Wilayani Mvomero, Shabani Hatibu (50) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa kutuhumiwa kumbaka binti yake wa kambo anayesoma darasa la tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Wilbroad Mutafungwa amesema, Septemba Mosi saa tatu asubuhi katika kijiji cha Madizini kata ya Mtibwa mkoani hapa, binti aitwaye Shadya Waziri (15), mwanafunzi wa shule ya msingi Mtibwa darasa la tatu, anadaiwa alibakwa na baba yake huyo wa kambo ambae ni fundi seremala.
Amesema, awali binti huyo alilalamika kwa mama yake mzazi aitwae Halima Issa (32) mkulima na mkazi wa Madizini, kuwa anasikia maumivu makali anapojisaidia haja ndogo na kueleza kuwa amebakwa mara mbili na baba yake wa kambo lakini alimtishia asiseme kwa mtu yeyote na endapo atasema basi angempiga.
Kamanda huyo amesema kuwa, taarifa walizopata zilidai kuwa, Agosti 30 wakati mama yake alipokuwa amesafiri kwenda msibani mjini Morogoro, na baada ya Polisi kupata taarifa hiyo kutoka kwa mzazi wa binti huyo walianza upelelezi na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo ambaye atafikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapokamilika.
More Stories
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya
Kenya,Uganda zaanzisha mradi wa uendelezaji rasilimali za maji Angololo