May 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yajue matumizi salama na sahihi ya Instagram yako kuepuka kufungiwa

Mwandishi: Ismail Mayumba

INSTAGRAM ni mtandao wa kijamii unaoruhusu mtumiaji kupata huduma ya kushirikisha picha za kawaida na za video mtandaoni.
Programu hii hutumika katika simu aidha za iPhone au mfumo uendeshaji wa Android.

Watu wengi mashuhuri wamewekeza kiasi kikubwa cha fedha na heshima zao na pia ni jukwaa la kuingiza kipato kwa kupitia matangazo.

Kutokana na sheria kali za usalama mtandaoni za Instagram imeleta taflani kwa wengi na kusababisha account zao zifungwe. Inakuwa hasara kubwa kwa wafanyabiashara kupoteza wateja wao, wanamuziki kupoteza wasikilizaji wao na vilabu kupoteza mashabiki zao. Kuunda account mpya mpaka kufika ulipoacha ni nguvu kubwa
sana inabidi itumike

Madhara Yanayosababishwa na Kufungiwa Kuzuiliwa mawasiliano ndani ya Instagram (communication restrictions).

Pindi utakapogundulika hatiani basi utazuiliwa Ku comment, ku-like, ku follow watu na hata pia utazuiliwa kuwasiliana na watu kwenye chats. Hii inaruhusiwa kuingia kwenye App ila umezuiliwa karibia asilimia 80 ya utumizi wa Instagram.

Adhabu nyingine ni kuzuiliwa ku post chapisho lolote mtandaoni. Hapa hutoweza kuleta mawazo yako mapya kwenye Mtandao mpaka wakufungulie matumizi ya kuchapisha machapisho

Unalazamishwa kutoka nje ya mfumo yani Forced Log out kinachofata wanataka uhakikishe kama ni wewe kweli mmiliki halali wa account unayotumia.

Adhabu hizi zinaweza kuja zote au moja inategemea na kosa umelifanya vipi. Kurudia kwa makosa kunaweza kusababisha ukafungiwa kabisa na usipate tena account yako.

Ni makosa yapi yanasababishwa kufungiwa kwa Account

Moja, kupuuzia warning au Alerts zinazoletwa na Instagram. Kwa mfano una like sana au una follow sana kwa kipindi cha muda mfupi na ukaletewa onyo . Ukipuuzia mara kwa mara basi hatasita kuchukua hatua

Mbili, taarifa ya kuhakiki account yako. Huwa inakujaga kama pendekezo na wengi wetu hupuuzia basi kupuuzia kwetu na ndo maana tunatolewa nje kwa lazima ili tuhakiki taarifa zetu

Kuacha matumizi hatarishi. Hii imebeba pointi nyingi Sana kama kutumia hashtags ambazo zimekatazwa, kuchapisha picha za uchi, kuchapisha machapisho ya chuki na kuchapisha kazi za watu.

Zote hizi na zinginezo husababisha account yako
kufungiwa Madhara ni madhara makuu na sababu ni sababu kuu ila zipo nyingi sana nikizidadavua kwa kina basi inabidi nitoe kitabu. Tuwe na matumizi salama ya Instagram ili kuepuka Kufungiwa account zetu