May 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wataalam Maendeleo ya Jamii waaswa kutoruhusu tamaduni potofu

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko amewataka wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kuhakikisha wanatekeleza Programu Jumuishi ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kwa kutoruhusu mambo na Mila zisizofaa kwa mtoto ili kutoathiri makuzi yao na Taifa kwa ujumla.

Aidha amewaasa wataalam hao kufanya kazi itakayowatambulisha katika maeneo yao ya kazi na kwa viongozi wao kwamba wapo na Wana umuhimu.

Dkt.Biteko ameyasema hayo jijini Dodoma Leo Mei 7,2925 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Alisema Serikali inayo Programu hiyo na kwamba inawategemea wao katika utekelezaji wake.

“Msikubali tamaduni zinazoharibu watoto ,pigeni kelele juu ya Malezi na Taasisi zinazokuja na tamaduni potofu na zisizofaa .”amesema Dkt.Biteko

Aidha kuhusu umuhimu wa wataalam hao alisema,mahali popote walipo,watu wengine wanapaswa kutambua kwamba upo usisubiri uambiwe wapo na siyo mpaka litokee tatizo ndipo uwepo wao uonekane.

“Wapeni ulazima Wakuu wenu kuwatafuta na kujua kuwa mpo,tena kupitia chama chenu furukuteni kwenye Halmashauri zenu na mahali mlipo ,na ninawaambia kwa uzoefu wa kawaida,tamko tu la kusema jamani sisi ni muhimu kama hamfurukuti, na mwakani tutakuja tutasema haya haya ,

“Usiruhusu mkubwa wako wa kazi mpaka aseme kuna kazi hii inafanywaa hivi ,ikifika baadaye ndiyo aseme kuna mtu fulani anaweza kuifanya,usifanye hivyo utakuwa umempa nafasi ya kukupuuza.”alisema Dkt.Biteko na kuongeza kuwa

“Ni kweli mpo kwenye muundo wa Halmashauri ,lakini kama mawakala wa maendeleo ya Nchi yetu hili ni kundi muhimu sana, fanyeni wote walio chini na juu yenu kujua taaluma yenu ni muhimu ,na ni muhimu kwenye kupanga maendeleo.”

Amewaasa wataalam hao kuwa miongoni mwa wanaopanga mipango ya maendeleo badala ya kuwekwa pembeni wakati huo muhimu.

“Msikubali wala msiruhusu kwamba wakati wa kupanga maendeleo ninyi muachwe nje ya ukumbi na wakati wa kutekeleza ndipo mtafutwe kuziba mapengo baada ya wengine kuonwa hawawezi kufanya hiyo kazi,

“Mfano ,utashangaa kukuta kwamba eti Afisa maendeleo ya Jamii yeye ndiyo muhamsishaji wa wananchi kujenga madarasa lakini wakati wa kupanga darasa lijengwe wapi aliwekwa nje ya ukumbi ,hiyo haikubaliki na lazima ninyi muwe na wivu na taaluma yenu.”alisisitiza Dkt.Biteko

Aidha amewahakikishia kuwa, Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali kwa kuanzisha Mpango wa Taifa wa kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa mwaka 2022/2023-2026 unaolenga kuwafanya wananchi kuwa kitovu cha maendeleo ngazi ya chini .

“Kwa hiyo mipango tuliyonayo ni lazima ianzie chini ambapo watekelezaji ni ninyi wataalam wa Maendeleo ya Jamii.” amesisitizaAwali ,Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima amesema mafanikio yaliyopo hapa nchini ni sehemu ya jitihada za Maafisa Maendeleo ya Jamii .