May 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Mkenda afungua mkutano wa 18 wa eLearning Afrika

Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amefungua mkutano wa eLearning Afrika ulioshirikisha Mawaziri wa nchi 20 katika Waziri  Kongamano la elimu ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere JNCC Dar es Salaam.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo ulioudhuliwa na Mawaziri 20 wa nchi za Afrika amesema lengo la mkutano huo kubadilishana mawazo na uzoefu jinsi ya kutumia Digital system kwa ajili ya sekta ya Elimu.

Prof.Mkenda amesema Tanzania inajitaidi kutumia Mfumo wa eLearning TEHAMA pamoja na kwamba hawajasambaza vya kutosha lakini pia kuna njia za kutosha kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yasio ya Kiserikali ili shule mbalimbali ziweze kufikiwa.

“Nchi yetu imepata heshima ya mkutano mkubwa wa 18 wa eLearning Afrika ulioudhuliwa na Mawaziri 20 kwa ajili ya kubadirisha mawazo pamoja  na uzoefu” alisema Profesa Mkenda

Prof.Mkenda amesema  watahakikisha shule nyingi zinafikiwa na mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kujifunza kompyuta ba walimu na walimu wote wapewe vishikwambi kwa ajili ya kusomea kwa sababu Rais wq Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alishatoa agizo wote wapatiwe vishikwambi.

Aidha amesema elimu mtandao wa kufundishia pia sisi wenyewe tuwe na teknolojia ya akili mnemba ambapo alisema Serikali imeruhusu shule kuanzishwa Zanzibar ya mfumo huo kuchukua wanafunzi watakaojifunza.

Pia amesema kozi kama hizo Chuo kikuu Dodoma na Nelson Mandela Arusha zinapatikana lakini bajeti ya mwaka huu wanafunzi wa kidato cha sita wanaofanya mtihani sasa hivi watapatiwa ufadhili wa masomo kama hayo.