Na Heri Shaaban (Ilala),Timesmajira
Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa wilaya ya Ilala kusimamia kampeni ya usafi.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema hayo katika kampeni ya usafi ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Dengu .
“Viongozi wa Serikali za mitaa katika halmashauri ya jiji la Dar es Salaam pamoja na wananchi naomba kuunga mkono kampeni ya usafi kila jumamosi kwenye mitaa yenu “amesema Mpogolo.
Mpogolo amesema ili kampeni hiyo iweze kuleta matokeo chanya ni vyema kila mmoja akatimiza wajibu wake kuhakikisha maeneo yote yanakuwa safi .
Aidha amesema wananchi wa wilaya ya Ilala wakijenga tabia ya kuwa wasafi watajilinda na kujikinga na magonjwa ya mlipuko hasa Kipindupindu hasa kipindi cha mvua hizi za masika zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali.

Katika hatua nyingine ameelezea umuhimu wa kutunza fukwe za Bahari pamoja na rasilimali za bahari zinazoweza kutumika kwa ajili ya maendeleo ya jamii na nchi ill kukuza uchumi katika nchi yetu.
Amewataka wafanye usafi katika ufukwe za bahari kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayochangia bahari kuharibika.
Katika kampeni hiyo ya usafi Wilaya ya Ilala Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Ellhuruma Mabelya aliwataka wananchi kuunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kampeni endelevu ya usafi .
Kampeni ya usafi Wilaya ya Ilala imewashirikisha Watumishi wa Halmashauri na Wakandarasi wa kampuni za usafi zoezi lilianzia makutano ya barabara ya kamata,kuelekea Utumishi,Teminal 1 kuelekea katikati ya mji na kumalizika katika eneo la dengu na fukwe za bahari ya hindi.
More Stories
Wazee wawili jela maisha kwa kubaka na kulawiti
Dkt.Biteko aongoza waombolezaji mazishi ya Mkurugenzi Mtendaji TANESCO
Nyongo: Sekta binafsi ina mchango mkubwa kwa taifa