Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, CPA. Amos Makalla, ametembelea daraja la Somanga lililopo mkoani Lindi na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ukarabati wa daraja hilo.
Daraja hilo ambalo limeharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni mkoani humo na kukata mawasiliano ya kati ya Dar-es-Salaam na Lindi.

Ambapo amesema,zaidi ya bilioni 100 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madaraja 13, mkoani Lindi ikiwemo daraja la Somanga, huku akimsisitiza Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega,kuhakikisha anasiamamia vyema wakandarasi ili madaraja hayo yajengwe kwa ubora na kwa hadhi inayostahili. na kusema kuwa fedha zipo za kutosha.
CPA Makalla amefika katika daraja hilo,Aprili 10, 2025 akiwa katika ziara yake ya kichama iliofanyika katika Mkoa wa Lindi na Mtwara, ambapo amempongeza Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, kwa weledi uliofanyika wa kurudisha mawasiliano kwa haraka katika daraja hilo huku akimtaka kuendelea kusimamia kwa ufanisi utendaji kazi katika daraja hilo.

Huku akimsisitizia kukemea uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji na kudai kuwa maendeleo yote yanayofanywa na CCM ni kwa maslahi ya wananchi.
More Stories
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya
Kenya,Uganda zaanzisha mradi wa uendelezaji rasilimali za maji Angololo