Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza utekelezaji wa mpango kabambe wa kuimarisha njia za kusambazia umeme na kuongeza ubora wa Nishati ya Umeme katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa kiTANESCO wa Kigamboni.
Mpango huu uliopewa jina la Umeme Bora Kigamboni umekuja baada ya maeneo ya baadhi ya maeneo ya Kigamboni kukumbwa na adha ya kukatika katika kwa umeme kulikosababishwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme pamoja na uchakavu wa miundombinu unaoathiri ufanisi wa utoaji wa huduma katika maeneo hayo.

Mpango huu unalenga kutekeleza Miradi 35 ya kuboresha ubora wa nguvu za umeme yaani (Voltage Improvement Project) na unatarajiwa kukamilishwa sambamba na matengenezo makubwa kwenye njia 8 (Feeders) za kusambazia umeme.
Akizungumza katika moja ya maeneo ambayo TANESCO wanatekeleza Mradi Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kifurukwe,Sultan Mbebe ameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kuanza utekelezaji wa miradi hiyo.
More Stories
Kakulima:Lushoto ni eneo muhimu kwa shughuli za utalii
Viongozi CHADEMA, Odinga wakutana, wajadili hali ya kisiasa nchini
Kamati ya Bunge yaridhishwa na ujenzi wa miradi kupitia mapato ya ndani