March 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi lamtia mkononi mtuhumiwa wa utekaji

Na Bakari Lulela,Timesmajira

JESHI la polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam, 8 machi 2025 lilimkamata mtuhumiwa Stanley Dismass Ulaya mkazi wa kata ya Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma kwa kumteka mtoto wa kiume ( 7) anayesoma kwenye shule iliyoko mbezi Dar es salaam.

Akizungumzia tukio hilo mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa jeshi hilo Jumanne Murilo amesema mtoto huyo alishushwa kwenye gari wakati akielekea shuleni nyakati za asubuhi na baba yake, ambapo jioni yake hakuweza kurudi nyumbani.

Baadae wazazi wa mtoto walifanya mawasiliano na walimu wake bila ya matumaini ya kumpata mtoto wao.

“Mtuhumiwa huyu alikuwa akipiga simu kwa wazazi wake kwa vitisho ambapo walikuwa wakihitaji pesa nyingi Ili wamrudishe kama wasipofanya hivyo atachukua hatua ya kumpoteza uhai wake,” amesema Kamanda Murilo

Aidha Jeshi la polisi kwa kutumia watalaalamu wake wa kiterejensia mtuhumiwa huyu alikamatwa maeneo ya Bagamoyo akiwa na yule mtoto na kupelekwa kituo cha polisi Osterbay.

Hata hivyo wakati taratibu zingine zikifanyika alitoroka na kukimbia ndipo polsi walipopiga risasi ya juu kama taharuki ambayo hakujali ndipo alipopigwa risasi ya miguu ambayo alikamatwa na kupelekwa hospitalni.

Kamanda amesema kuwa hali ya mtoto aliyetekwa inaonekana kuwa njema na taratibu nyingine za kumchunguza zinaendelea.

Jeshi la polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linaendelea kulaani vitendo vyote vinavyohusiana na masuala ya utekaji unaohatarisha maisha ya wanajami