Na Mwandishi wetu,Timesmajira
KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita kupitia sekta ya Kilimo Kampuni ya Mzuri Afrika na Agrami Afrika wamekuja na Teknolojia ya MZURI (Mashine) ambayo imelenga kuwasaidia wakulima kulima kilimo cha kisasa na chenye tija.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam janaleo Machi 7, 2025 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Shaaban Mgonja amesema Kampuni hiyo imeamua kuja na teknolojia hiyo ambayo imelenga kuleta Mapinduzi katika sekta ya kilimo
” Teknolojia ya MZURI (Mashine) imekuja kuleta Mapinduzi ambayo yatalahisisha shughuli za kilimo shambani kwani asilimia 60 ya watanzania ni wakulima”amesema
Amesema teknolojia hiyo katika Afrika ipo katika Nchi 50 ikiwemo Tanzania huku asilimia 30 ya Ngano inayolishwa nchini Ukraine ikizalishwa kupitia Teknolojia hiyo.
Akitaja faida za Mashine hiyo amesema inauwezo wa kulima, kulegeza ungo, kuchanganya mbolea na kuweka mbegu ardhini,.
“Tunazo mashine za aina tatu, tuna ya mita 3 ambayo inauwezo wa kulima eka saba kwa saa, tuna ya mita nne na Mita sita, Teknolojia hii inauwezo wa kurahisisha sana shughuli za kilimo,” amesema Mgonja.
Pia amesema Teknolojia hiyo inauwezo wa kupanda mazao jamii ya nafaka pekee.
Aidha ameeleza kuwa kupitia Teknolojia hiyo Kilimo tayari wanashamba la ekari 300 Vigwaza mkoani Pwani ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kulima ufuta ekari 200 Kwa kutumia Mashine hiyo
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mzuri World Marek Rozniak amesema kuwa wameamua kuja na teknolojia hiyo kwa watanzania kulima kilimo cha kisasa na chenye tija.
” Teknolojia hiyo itasaidia kuongeza uzalishaji wa Ngano nchini kwani kwa asilimia zaidi ya 90 ya Ngano inayotumika Nchini imetoka nje ya nchi”amesema Rozniak
More Stories
Prof.Muhongo aipatia mifuko 50 ya saruji kamati ya ujenzi Sekondari ya Mmahare
Mgao wa tenda wa 30% kwa makundi Maalum ,wamkosha Rais Samia
Umoja wanawake Chuo cha Magereza Kiwira watoa msaada kwa wazee