March 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania watakiwa kudumisha amani

Na Bakari Lulela ,Timesmajira

WAZIRI mkuu Kassimu Majaliwa amewataka watanzania kuwa na umoja katika kudumisha uhuru, amani na utulivu katika kuliombea Taifa.

Kauli hiyo amesema jijini Dar es salaam kwenye  viwanja vya Leader s Club kongamano maalumu la kuliombea amani Taifa huku tukielekea kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu nchini kote.

“Kwa umoja huu ninawaomba umma wa watanzania kuzidi kuliombea amani Taifa letu na kuwaombea viongozi wetu waweze kusimamia maombi yetu mbele ya mungu,” amesema Majaliwa

Aidha Majaliwa ameeleeza kuwa Sote  tumekuja mahala hapa kwa utulivu wa amani na mungu ataturudisha majumbani kwetu kwa amani Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio aliyekuwa mgeni rasmi mahala hapa lakini ameniagiza nifikishe salamu hizi kwa umma huu.
 
Maaskofu wote Leo nimepata faraja sana kwa kukutana nanyi na viongozi wote mlio kusanyika  hapa siku ya Leo ni muhimu sana. hakika sikutarajia kukuta umma wa watanzania mahala hapa ni mshikamano mkubwa katika Taifa letu.

Nawathibitishia viongozi wa dini kuwa Serikali ilpo pamoja na viongozi wa dini hivyo serikali yenu iinawapenda na kuhakikisha viongozi wetu wanatupenda 
Zaidi ya viongozi wa dini walishiriki Ili kuliombea Taifa hili liweze kupitia salama ktk uchaguzi mkuu unaotarajia kifanyika mwezi Novemba mwaka huu

Tumeona baadhi ya maeneo yenye changamoto ya maji ,umeme lakini kutokana na maombi yenu nchi hii imebarikiwa.
Kuna huduma muhimu ambazo mlizitoa katika kuwahudumia wananchi pasipo kubagua dini, rangi wala kabila .

Huduma mbalimbali zimetumika katika kuhudumia watanzania Ili kupata wepesi na usalama ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Barabara za rami, mabwawa ya maji ambapo tumejenga bandari na viwanja vya ndege.

Nyinyi ni mashahidi katika masuala la maridhiano hlvyo jukumu kubwa katika kuliombea Taifa hili na kuzidi kuuombea amani uchaguzi mkuu 

Nitoe wito muendeleee kuiombea amani nchi yetu na kumuombea Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassani na kumuombea Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi
Mungu aweze kuwapa afya njema ya kuwatumikia watanzania.