Na Penina Malundo,Timesmajira
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki Tanzania, Ado November, ametangaza rasmi uzinduzi wa Tuzo za Muziki wa Injili Afrika Mashariki.
Huku Serikali ikiwa tayari kushirikiana na waandaaji wa Tuzo hizo na kusaidia kufika mbali zaidi katika kuhakikisha vipaji vya wanamziki vinazidi kufika mbali zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa Tanzania imeshirikiana na East Africa Gospel Awards,(EAGMA) zikihusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, na Sudani Kusini.
Ado November ameongeza kuwa tuzo hizo zitakuwa faraja kwa wasanii wa muziki wa Injili nchini Tanzania, kwani jitihada zao za muda mrefu sasa zinakwenda kuleta matunda.
“Muziki huu sasa utwafuta machozi wasanii wetu baada ya kuufanya
kwa muda mrefu, lengo la tuzo hizi ni kuwaleta pamoja wanamuziki wa injili ambao wanafanyakazi kubwa katika kuelimisha na kuburudisha jamii yetu kwa ujumla,” amesema.
Aidha amesema tuzo hizo zinatarajiwa kuinua na kuthamini mchango wa wasanii wa Injili katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku zikitoa jukwaa la kuutangaza muziki wao kimataifa.

Awali akiongea wakati wa uzinduzi wa Tuzo hizo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Dkt.Emmanuel Ishengoma amesema tuzo hizo ni za kihistoria kwa sababu zinafanyika kwa mara ya kwanza hivyo ni vema kuhakikisha zinasimamiwa kikamilifu katika kuhakikisha zinakuwa endelevu.
“Mawazo yenu yawe ya muda mrefu yanayotekelezeka na yanadumu,kumuimbia Mungu ni kusali mara mbili, hivyo waliojitolea kumuimbia Mungu wanatusaidia kusali mara mbili,”amesema
Amesema wazo hili la uwepo wa Tuzo hizo lisiangalie tu kwa nchi za Afrika Mashariki pekee ila liende mbali zaidi kwa nchi zote za Afrika.

Kwa upande wake Muandaaji wa Tuzo hizo EAGMA,Magreth Chacha amesema EAGMA inaunganisha wasanii,mashabiti na wataalamu wa sekta ya muziki kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Amesema madhumuni ya muanzisha tuzo hizi ni pamoja na kuvuna nafsi kwa kristo kupitia nguvu ya muziki wa injili hasa kwa vijana ambao mara nyingi wanapotea kwenda kuimba muziki wa kidunia.
“Tunajitahidi kutengeneza muziki wa kuleta mabadiliko ya kudumu katika kusherehekea vipaji vya muziki wa dini.
“Tukio hili la Tuzo za Injili kwa nchi za Afrika Mashariki ni tukio la matumaini hamasa na imani zinazokutana katika kusherehekea nguvu za muziki wa injili,”amesema.
More Stories
Katibu Mkuu Nishati aipongeza Sweden kufadhili miradi ya umeme nchini
RAS Seneda akabidhi msaada wa Mablanketi kwa wazee na yatima
Balozi Nchimbi:Mapambano ya uhuru wa kiuchumi Kusini mwa Afrika yanaendelea