February 28, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mulugo atoa rambirambi familia nne zilizopoteza wapendwa kwa ajali

Na Esther Macha, Timesmajira Online,Mbeya

MBUNGE wa Jimbo la Songwe ,Philipo Mulugo amefika jijini Mbeya kushiriki na kuaga miili ya watu wanne waliofariki kwenye ajali akiwemo mwandishi wa habari na mpiga picha wa TBC Furaha Simchimba.

Watu hao waliofariki katika ajali iliyotokea Februari 25,2025 iliyohusisha gari la kampuni ya CRN Safari na gari la Serikali aina ya Land Cruiser.

Mulugo akitoa salamu hizo pia amekabidhi rambirambi kwa familia nne zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo .

Waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Daniel Mselewa, Thadeo Thadeo, Isaya Geazi na Furaha Simchimba.