February 28, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Huduma kwa wateja EWURA sasa kidigitali

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Dodoma


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imezindua mfumo wa kidigitali wa utoaji huduma kwa wateja ambapo watoa huduma watakuwa wakipokea mawasiliano ya simu kupitia kompyuta mpakato.

Awali mpokeaji wa simu alitakiwa kuwa na simu ya mezani,huku namba ya huduma kwa wateja itakayokuwa inatumika kupiga simu bure ni 0800110030.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile, Februari 27,2025,amezindua mfumo huo kwa kuhudumia wateja moja kwa moja waliopiga simu kufahamu masuala mbalimbali ya kiudhibiti kwenye sekta zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo za nishati na maji.

“Tunapozindua mfumo huu wa kidigitali, iwe chachu kwetu kutoa huduma kwa wateja kwa ufasaha na ufanisi zaidi na popote ambapo mtoa huduma atakuwepo ulipo mtandao,”amesisitiza.