February 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kapufi :Uimarishaji huduma za afya  umepunguza matibabu ya nje ya nchi

Na George Mwigulu,Timesmajiraonline,Dar

MWENYEKITI  wa chama cha kibunge cha idadi ya watu (TPAPD) na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Sebastian Kapufi, ameeleza kuwa upatikanaji wa vifaa vya kisasa na huduma bora katika sekta ya afya umechangia kupunguza idadi ya Watanzania kwenda kupata matibabu nchini India.

Kapufi akizungumza Februari 25, 2025  katika Mkutano wa Wabunge wa Afrika na Asia juu ya idadi ya watu na maendeleo, amesema ongezeko la watu linapaswa kwenda sambamba na utatuzi wa changamoto zinazosababishwa na athari la ongezeko la watu kwa kutoaji huduma bora za afya jambo ambalo limefanyika hapa nchini.

Mkutano huo ambao wabunge wamejadili kuunganisha takwimu za idadi ya watu ili kukuza ujumuishaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, Kuunganisha mgawanyiko wa idadi ya watu na matarajio ya changamoto za athari ya idadi kubwa ya watu wasiozalisha na ukosefu wa ajira, uwezeshaji wa wanawake na wasichana kuchochea maendeleo endelevu, kuwekeza katika fursa za vijana na ajira na kufanya jukumu la kuziba mapungufu ya sheria.

Mwenyekiti huyo wa TPAPD akiwa jijini Dar es salaam, Amesema hapa nchini uboreshwaji wa huduma za afya hosptali ya Muhimbili na uimarishwaji wa huduma hospitali ya Amana na Mwananyamara umeondoa kero ya watu kutafuta matatibabu nje ya nchi ambapo umeakisi  uuganishaji wa idadi ya watu kwenye kukuza maendeleo ya jamii.

Amesema akitoa mfano kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu  na makazi ya mwaka 2022 hapa nchi kuna jumla ya idadi ya vijana zaidi ya milioni 21 sawa na asilimia 34 ya watu zaidi ya milioni 61 huku wazee wakiwa ni milioni tatu sawa na asilimia tano ya watu wote ambapo kimsingi ni tegemezi na serikali inajukumu la kuweka mazingira bora za huduma.

Amesema ukiwa na jamii ambayo haina afya bora mambo yote yanayopangwa kufanywa yanakosa maana jambo ambalo serikali imefanya kazi nzuri na kubwa ya kuimarisha eneo hilo la afya  kwa kujenga kila pembe ya nchi zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Akizungumzia athari la ongezeko la watu ulimwenguni, Kapufi amefafanua kuwa TPAPD imeona mtoto wa kike kwa namna gani anaweza kunusuliwa na mambo mbalimbali ili aweze kushiriki kwenye uchumi wa nchi huku wakiangalia idadi ya watu kuweza kuwa neema na siyo balaa.

Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Afrika Kusini Pemmy Majodina, amesema kuwa Bara la Afrika limeathiliwa na mimba za utotoni nani vigumu kudhibiti kama idara ya afya na hosptali bali inategemea wazazi na jamii kuona ni nini cha kufanya kujenga jamii  sio ya kutibu dalili bali kuwa na jukumu la kuzuia kama wazazi na wategeneza sheria na sera.

Majodina ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kuwekeza zaidi katika taasisi za afya kwani uwekezaji kwa watu maana yake ni kuwekeza kwenye afya.

“Leo hapa tunadhibitisha kwamba tunachukua jukumu la afya mikononi mwetu kwa sababu uzaishaji wa taifa unategemea taifa la Tanzania lenye afya” amesema.