Na Esther Macha, Timesmajira Online,Mbeya
Imeelezwa kuwa uanzishwaji wa kampeni ya msaada wa kisheria kwa wananchi inayoitwa Mama Samia Legal Aid Campaign,itatoka suluhisho kwa kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya ya malalamiko kwenye Mahakama.
Hayo yameelezwa Februari 24,2025 na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya,Suma Fyandomo, wakati alipowawakilisha Wabunge wa Mkoa huo kwenye ufunguzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign uliofanyika uwanja wa Kabwe jijini hapa.
“Rais Samia ameutazama Mkoa wa Mbeya kwa jicho la upendo,ambalo linaenda kutoa suluhisho la malalamiko kwa wananchi na kuwa msaada,hivyo nimpongeze kwa hatua hii aliyofanya,”amesema Fyandomo.
Amesema Rais Samia amethubu kuanzisha kampeni hii ya msaada wa kisheria kwa wananchi wasio na uwezo wa kuweka Mawakili kutokana na kukosa fedha ili waweze kusimamia kesi zao.
Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid Campaign itafanyika mkoani Mbeya siku 15.
More Stories
TAKUKURU Gairo waja na kliniki tembezi kutoa elimu ya kupambana na Rushwa
Said :Miundombinu ya maji mkunduge mambo safi
Wadau wakutana kwa tathimini maendeleo ya Elimu