Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
MAMLAKA ya Elimu Tanzania(TEA)imesema imetenga bilioni 3.0 kwajili ya kuimarisha miundombinu ya utoaji wa mafunzo ya amali ili kufanikisha utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Februari 25,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa TEA,Dkt.Erasmus Kipesha wakati akizungumza na waandishi wa habari utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo katika miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.
Ambapo amesema shule 20 zitanufaika na mpango huo zikiwemo shule za Sekondari zinazotoa mafunzo ya ubunifu na ufundi stadi.
Aidha Dkt.Kipesha amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/25 TEA imepanga kufadhili jumla ya miradi 113 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule za msingi na Sekondari kwenye maeneo mbalimbali nchini yenye thamani ya sh.bil.11.3.
“Miradi hii itakapokamilika itanufaisha wanafunzi 29,482 na walimu 12 katika shule za msingi na sekondari,miradi hii inajumuisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 45 pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa 11,matundu ya vyoo 336,nyumba za walimu 12,mabweni 8 na ununuzi wa vifaa vya TEHAMA kwa shule 9.
Pamoja na hayo TEA imesema katika kipindi cha miaka minne ya awamu sita,Mamlaka hiyo imepokea jumla ya Sh.bil.49.05 kutoka serikali kuu kwa ajili ya mfuko wa Elimu na jumla ya sh.bil.3.8 kwajili ya mfuko wa kuendeleza ujuzi.


More Stories
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani
Taarifa za maendeleo ziwafikie wananchi kwa usahihi
Apps and Girls, Yas Waadhimisha Mahafali Wahitimu wa Jovia 2025