February 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Exim bank yaingia mkataba wa Zati

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Benki ya Exim imeingia mkataba wa miaka mitatu na Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI) kwa lengo la kukuza na kuinua sekta ya utalii Zanzibar. Mkataba huo ulisainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Fedha kutoka benki ya Exim, Shani Kinswaga pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI), Suleiman Ally, ukishuhudiwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mudrick Soraga