NA HERI SHAABAN( ILALA)
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, ametoa mifuko kumi ya Saruji katika shule ya elimu ya Lukema iliyopo wilayani Ilala.
Msaada huo Meya Kumbilamoto alitoa Dar es Salaam jana,kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye upande wa sekta ya elimu ili Taifa letu liweze kupata wataalam na wasomi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
“Nimetimiza ahadi yangu katika Nusery ya Lukema kwa kukabidhi mifuko kumi ya saruji kwa ajili ya kutatua changamoto katika nursery hii ya Lukema saruji hii mtaitumia katika kuboresha miundombinu ya nursery yenu “alisema Kumbilamoto .
Meya Kumbilamoto alisema wilaya Ilala, ina shule zaidi ya 200 na kiwango cha ufaulu kila mwaka kinaongezeka kwa shule hizo kufanya vizuri kitaaluma.
Amewataka Wazazi kushirikiana na Walimu katika kufatilia maendeleo ya wanafunzi shuleni kila wakati kwa ajili ya kumjengea mazingira bora mwanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule Lukondo Machunde,amemshukuru Meya Kumbilamoto kwa kukabidhi saruji hiyo watakayotumia kuboresha miundombinu ya shule .
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Vingunguti naye alitumia fursa hiyo kumshukuru Meya Kumbilamoto misaada hiyo anayo toa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani.
More Stories
Wanawake Kisukuru kuwezesha kuku kujiinua kiuchumi
21 washikiliwa kwa tuhuma mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa mtaa, kitongoji
Wananchi wamuunga mkono Prof.Muhongo uvuvi wa vizimba