Ashura Jumapili,TimesMajira Online,Bukoba
Upungufu wa viti na meza 350, shule ya sekondari Bakoba,iliopo Kata ya Bakoba Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba,inawafanya wanafunzi kuandika kupitia migongo ya wenzao au mapajani.
Hali hiyo inamyima usingizi,Diwani wa Kata ya Bakoba Shaban Rashid,ambaye amesema mbali na wanafunzi kukutana na changamoto ya kukosa sehemu ya kuweka daftari wakati wa kuandika,walimu pua wanakutana na miandiko mibaya.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0006.jpg)
Rashid,amesema hayo Februari 11,2025 katika kikao cha wadau wa elimu wa Kata hiyo,chenye lengo la kuangalia namna bora ya kutatua changamoto za elimu katika Kata ya Bakoba na kupunguza ufaulu hafifu.
Ambapo,amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo, Kamati ya Maendeleo ya Kata,imeamua kuvuna miti iliyokuwa ofisi ya Kata na kupata meza na viti 50, ambavyo tayari wamekabidhi kwenye shule hiyo.
Pia amesema,changamoto nyingine ni kushuka kwa taaluma katika shule ya sekondari Bakoba hasa matokeo ya kidato cha nne na kidato cha pili, na jamb hilo linachangiwa na ushiriki duni wa wazazi katika mipango ya walimu ya kuboresha kiwango cha taaluma.Kwani wanapoitwa kwenye vikao vya shule hawahudhurii.
“Shule ina wanafunzi zaidi ya 700 lakini wazazi waliofika kwenye kikao ni chini ya 30.Desemba, 2024 walimu waliamua kuzuia matokeo ya watoto ili wazazi waweze kufika shuleni,lakini Januari mwaka huu matokeo ya watoto 300 yalikuwa hayajachukuliwa na wazazi,”.
Huku akisisitiza kuwa vikao vya wazazi na walimu ni muhimu kwa maslahi ya wanafunzi na jamii kwa ujumla, kwa kuinua kiwango cha elimu.
Hata hivyo amebainisha kuwa changamoto nyingine ni upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi katika shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima,amesema changamoto nyingine za shule wazazi kwa kushirikiana na walimu wanaweza kuzitatua hivyo wazazi wasimame katika nafasi zao.
Sanjari na hayo Sima,amewaonya wazazi wanaopeleka watoto wao wenye ulemavu shule ya msingi Mugeza mseto,waache kuwatelekeza na badala yake wawatembelea ili kujua maendeleo yao sambamba na kushiriki vikao vya shule.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0005.jpg)
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa, amesema wazazi waachane na uchawa ni matokeo ya ufukara wa akili na badala yake wapeleke watoto shule.Kwani wanaowafanyia uchawa watoto wao wanasoma shule nzuri na hawawezi kuwa machawa.
“Acheni uchawa somesheni watoto suala la kumpa mtoto chakula ni lazima sio hiari,ni huduma ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao,”amesema Hajath Mwassa.
Amebainisha kuwa siri ya kufanya vizuri katika masomo na kufaulu,inatokana na uhusiano baina ya mwalimu na mwanafunzi na kama mwanafunzi ana njaa hawezi kusikiliza vizuri na kumuelewa mwalimu.
Pia amesema silaha ya mtoto wa kike ni kusoma sio kufundishwa kupika pilau,zama zimebadilika kwani wanaume wa siku hizi wanataka mwanamke.anayeweza kuchangia kipato kwenye familia.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0004.jpg)
More Stories
Wasira ‘aipiga nyundo ‘No reform no election
Tabora wapongeza uimara wa CCM
CCM yahimiza uadilifu kwa watumishi manispaa Tabora