Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara Edward Ole Lekaita ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya kuweka mpango wa kuwafikia wastaafu walipo ili kupata huduma muhimu kama za NHIF.
Mbunge Lekaita ameyasema Februari 7, 2025 wakati alipouliza swali Bungeni kupitia Wizara ya Afya,ambapo amesema wazee wastaafu wamekua wakipata tabu kusafiri kutoka walipo hadi Dodoma,kwa ajili ya kuhakiki taarifa zao za NHIF.
“Kwanini msiweke mpango muwafikie hawa wastaafu maeneo walipo wajikusanye na kuwapa taarifa maalum? alihoji Mbunge Lekaita.
Aidha akijibu hoja hiyo Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel amesema,”Mbunge Lekaita aliandika barua kwenda Wizara ya Afya, akiomba Wazee wasije hapa Dodoma, ama kwenda ofisi za Mikoa kuhudumiwa kule. Tumeiona barua yako,sasa wale wazee wastaafu wa Kiteto wakusanye na wataalam watawafuata huko na itakua hivyo kwa Wabunge wote,”.
More Stories
Dkt.Kiruswa:Madini ya Tanzanite kuuzwa kwenye masoko ya ndani,nje ya Mirerani
Chalamila ataka jamii kutafsiri kwa vitendo maendeleo yanayofanywa na Rais Samia
Wassira:CCM tutashinda dola kwa kura,si bunduki