Na Penina Malundo,Timesmajira
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania Balozi Mohmoud Thabit Kombo amesema Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) waliokutana leo unalengo la kuleta matokeo chanya juu ya mapigano yanayoendelea katika mji wa Goma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo uliowajumuisha mawaziri kutoka nchi wanachama wa EAC na SADC,Balozi Kombo amesema msimami wao ni kuandaa njia sahihi ya kutafuta suluhu ya kudumu kama inavyotambua nyimbo za Taifa na kikanda.
Amesema lengo la kukutana mawaziri hao ni kutafakari na kutafuta suluhisho la pamoja kwa kanda zote mbili za SADC na EAC.
“Tunapokutana leo tunafahamu mchakato wa kudumu wa upatanishi wa kikanda juu ya utatuzi wa mzozo wa DRC, Rwanda kupitia mazungumzo ya Nairobi na ya Luanda yaliyoongozwa na Rais wa Angola João Lourenço na Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ukiendelea kupata suluhu ya amani.
“Hali ya usalama wa Congo inabaki kuwa tete na kuhatarisha haki za binadamu hivyo ni lazima kupitia mkutano huu tupate suluhisho la kudumu,”amesema Balozi Kombo
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa SADC, Elias Magosi amesema hali ya kiusalama bado tete kusababisha maafa kwa wanajeshi wanaotoa msaada ya kibinadamu kwa wanawake,wazee na watoto ambao ni waathirika wakubwa.
Amesema mkutano huu umekuja baada ya mkutano wa dharura wa Wakuu wa nchi uliofanyika nchini Harare,… katika kutafuta suluhu ambapo SADC imekuwa ikifanya mikutano ya kidplomasia.
“Mkutano huu ni muhimu sana kwani takribani miaka 30 tangu mgogoro huu kuanza hali inayofanya watu wa Congo kuwa na mashaka katika kupatikana kwa suluhu.
“Mkutano huu wa pamoja utaleta mapendekezo yatakayoleta mipango ya utekelezaji na kikomo cha uwepo wa mgogoro huu kwani bila kuonyesha vielelezo hivi itaonekana mkutano haujazaa matunda,”amesema.
Amesisitiza kuwa lazima walete muafaka kwani hali bado ni tete wananchi wa nchi hiyo.
Naye Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva
amesema kupitia mkutano huo utakuwa na msingi wa kuleta makubaliano ambayo yataleta matokeo yanayotekelezeka kwa nchi za Afrika.
“Mkutano huu ni muhimu kwani umeitwa kwa muda mfupi na majadiliano yetu yaangalia jirani yetu,tunajukumu kama jumuiya kuja na maazimio ya pamoja tayari tumefanya mikutano kadhaa kujadili usalama wa DRC ni kuleta amani,”amesema.
“Sisi kama sektarieti tumefatilia mkutano wa wakuu wa nchi tuliazimia kuja na mkutano huu wa pamoja ambao utakuwa msingi wa kuleta matokeo mazuri,”amesema.
More Stories
Kilosa waanza kuonja asali ya hewa ukaa
Maadhimisho siku ya Kimataifa ya Wanawake na wasichana katika sayansi kufanyika Dodoma
Watanzania wakumbushwa kudumisha na kulinda amani