Na Joyce Kasiki, Timesmajira online,Dodoma
MBUNGE wa Kilombero Abubakari Asenga ameihoji Serikali kwamba lini itawalipa fidia wananchi waliopisha barabara ya mchepuko kutoka Ifakara, Kikwawila, Mbasa hadi Lipangalala.
Asenga pia amehoji swali hilo Februari 7,2025 Bungeni jijini Dodoma katika kipindi Cha maswali ambapo pia ametaka kujua hatma ya wananchi hao ambao wamekuwa wakisubiri kwa zaidi ya miaka sita sasa bila kulipwa fidia.
Aidha katika hatua nyingine ameitaka kujua ni lini wananchi waliopisha ujenzi wa barabara ya Ifakara -Kidatu watalipwa fidia kwani tathimini imeshafanyika.
“Katika barabara ya Ifakara Kidatu ambayo Rais Samia Suluhu Hassan alizindua Agosti mwaka Jana tathimini imeshafanyika imegundulika kuna wananchi bado wanadai kihalali ,hawa nao watalipwa lini fidia zao?amehoji Asenga
Akijibu maswali hayo,Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema
Serikali imekamilisha Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Awali wa barabara ya Mchepuo wa Mji wa Ifakara yenye urefu wa kilometa 10 huku akisema ,kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Sambamba na hilo Mhandisi Kasekenya amesema,taratibu za kufanya tathmini za mali zote zitakazo athiriwa na ujenzi zinaendelea na mara baada ya kukamilika kwa tathmini hiyo,Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wote waostahili kwa mujibu wa sheria.
Aidha amekiri kwamba ni kweli kwamba tathimini ya barabara ya mchepuo ya Ifakara ilifanyika muda mrefu.
“Ni kweli kwamba tathimini ya barabara hii ilifanyika muda mrefu na ndio maana kinachofanyika hivi sasa ni kuihuisha ..,hii barabara ilitakiwa ijengwe mapema maana kwa sababu ya ukuaji wa mji wa Ifakara barabara iliyopo katikati imekuwa haitoshelezi mahitaji ya mji huo kwa sasa.”amesisitiza Mhandisi Kasekenya
Kuhusu wananchi waliopisha barabara ya Ifakara Kidatu Mhandisi Kasekenya amesema wale wote waliokuwa wanastahili kulipwa kwa mujibu wa Sheria walilipwa .
“Lakini pia Kamati inayoshughulikia malalamiko chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero ilionekana wengine pia waliathirika kutokana na ujenzi ambao ama barabara ilisogea ama baada ya kukata magema walionekana waliotakiwa waondoke kwa hiyo walitakiwa kulipwa,tayari tulishapokea taarifa zao ambapo baada ya kupitia taarifa ya Kamati inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya wanastahili walipwe ,hivyo wananchi hao,watalipwa hizo fidia zao.
More Stories
Mbaruku:Lushoto haikutakiwa kuwa na shida ya maji
Mawaziri wa EAC,SADC wakutana Dar kujadili usalama wa Congo
Lukuvi awataka watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kuyafikisha mafanikio ya utendeji wa Ilani ya CCM kwa wananchi