![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Screenshot_20250207-0959552.jpg)
Na Joyce Kasiki,Dodoma
SERIKALI imejipanga kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda kwa ajili ya uchakataji wa mazao ya wakulima hususan yale yanayoharibika haraka Ili wakulima hao wasipate hasara.
Hatua hiyo imelenga kuokoa mazao yanayoharibika kwa haraka mashambani kama vile chai na parachichi na kusababisha wakulima kupata hasara,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma February 6 ,2025 wakati akijibu awali la Mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda wakati wa maswali ya papp kwa papo kwa Waziri Mkuu .
Awali katika swali lake,Mwakagenda alitaja kujua kwa nini Serikali isitoe agizo kwa wawekezaji wanaonunua mazao ya Parachichi na Chai waweze kuyanunua kwa wakati badala ya kuacha mpaka yaharibike.
“Kunekuwa na baadhi ya mazao yakipata bei nzuri na yakisaidia wakulima kupata mahitaji ,lakini kunekuwa na mwenendo mbaya kwa wawekezaji na baadhi ya wanunuzi hawafanyi vizuri kwa wakulima hasa yale mazao yanayoharibikia shambani,
“Nini mkakati wa Serikali kusema na kutoa agizo kwa wawekezaji na baadhi ya wanunuzi kuhakikisha wananunua mazao hayo kwa wakati ikiwemo parachichi na chai kwani wamekuwa wakichelewa kwa makusudi ili bei iweze kushuka kwani hapo wakulima wanakaribia kupata hasara.?”alihoji Mwakagenda
Majaliwa alisema Serikali imejikita katika kusimamia kilimo nchini, kilimo ambacho kinatoa mazao ya biashara na chakula na manufaa na sasa inaenda kujikita katika uchakataji ili kilimo kiwe na tija.
Alisema katika usimamizi huo wa mazao ya biashara Serikali inatambua kwamba zipo changamoto ikiwemo mazao mengine yanayoharibika kwa haraka na hivyo kuuzwa kwa bei ya chini.
“Mkakati wa Serikali ni kwamba tutahakikisha mazao haya tunayawekea utaratibu ambao ndani ya Serikali tumeamua kuweka Mamlaka / Bodi zinazosimamia mazao kuanzia uratibu tangu kwenye Kilimo
ili kuokoa mazao hayo ,kwanza tumehamasisha uwekezaji kwenye viwanda ili tuweze kuchakata mazao haya kwa lengo la kuyafanya yasifikie hatua ya kuharibika,
na kwa kuchakata tutapata bei nzuri lakini pia mkulima anapata mazao mengi.
More Stories
Kampuni ya ununuzi wa tumbaku yarejesha faida kwa jamii
Waziri Slaa:Anwani za makazi zinarahisisha upokeaji na utoaji huduma
Rais Samia awaonya Majaji na Mahakimu