February 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

EWURA yatangaza bei kikomo za mafuta

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano ya Februari 5, 2025 saa 6:01 usiku,katika taarifa yake kwa umma ilioyolewa Februari 5, mwaka huu.

Kwa mwezi Februari 2025, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.Ambapo kwa bei kikomo za rejareja Bandari ya Dar-es-Salaam petroli lita moja itauzwa kwa Tsh 2,820,dizeli Tsh. 2,703 na mafuta ya taaTsh. 2,710, Tanga petroli Tsh.2,825,dizeli Tsh. 2,749 na mafuta ya taa Tsh. 2,756 huku Mtwara petroli Tsh.2,892,dizeli Tsh. 2,775 na mafuta ya taa Tsh. 2,782.

Huku bei kikomo za jumla Bandari ya Dar-es-Salaam lita moja petroli itauzwa kwa Tsh.2,689.46, dizeli Tsh.2,572.11 na mafuta ya taa Tsh.2,579.99,Tanga petroli Tsh.2,694.63 na dizeli Tsh.2,581.71 na Mtwara petroli Tsh.2,700.54 na dizeli Tsh.2,590.85.

Taarifa hiyo imesema,bidhaa za mafuta zinazoagizwa na kupokelewa hapa nchini zinazingatia bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) kutoka soko la Uarabuni.

Ambapo Februari 2025, bei kikomo za mafuta zimekokotolewa kwa kuzingatia bei za mwezi Januari 2025. Ikilinganishwa na Desemba 2024, bei za Januari zimeongezeka kwa asilimia 3.82 kwa mafuta ya petroli,asilimia 6.77 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 5.87 kwa mafuta ya taa.

Pia gharama za uagizaji mafuta (Premiums) zimepungua kwa wastani wa asilimia 4.90 kwa petroli, asilimia 14.94 kwa dizeli na wastani wa asilimia 0.81 kwa mafuta ya taa.