February 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wiki ya Sheria yatambua mchango wa Majira, TimesMajira Online

Ashura Jumapili TimesMajira Online, Bukoba,

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba iliyopo mkoani Kagera imetoa cheti cha kutambua mchango wa gazeti la Majira na TimesMajira Online kwa kazi iliofanya ya kuhabarisha umma katika wiki ya sheria .

Cheti hicho kimetolewa na mgeni rasmi katika siku ya sheria nchi Februari, 3 mwaka huu,Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Bukoba Immaculata Banzi katika viwanja vya mahakama hiyo Bukoba Manispaa.

Jaji Banzi,amesema katika maadhimisho ya wiki ya sheria walifanya kazi na vyombo vya habari 41 na Gazeti la Majira na TimesMajira Online imekuwa sehemu ya kuwafikia wananchi milioni 15.9 waliopewa elimu kuhusu mada mbalimbali za kisheria.

Wakati akikabidhi tuzo hiyo kwa mwakilishi wa gazeti la Majira na Timesmajira Online koani Kagera, Ashura Jumapili,Jaji Banzi ametoa pongezi kwa chombo hicho kujitoa kuhabarisha umma, juu ya elimu iliyotolewa katika makundi mbalimbali ya kisheria.